Poetry

Drop Your Poem Here

12 comments:

  1. BINADAMU

    Binadamu sio mtu, hakika ninakubali,
    Kwake yeye hana utu, mabaya yake halali,
    Atakujazia kutu, sipotumia akili,
    Kwanini binadamu, una moyo kama sumu?

    Mazuri kimfanyia, kwake aona upuzi,
    Heshima kimpatia, akuona kama mbuzi,
    Sijaribu sogelea, takutemea kohozi,
    Kwanini binadamu, una moyo kama sumu?

    Binadamu hana wema, usije mfuatilia
    Takupoteza mapema, shimoni kukutupia,
    Na maneno atasema, huwezi kushindania,
    Kwanini binadamu, una moyo kama sumu?

    Binadamu kama samba, mwituni kajikalia,
    Tasikia akiimba, viswala navingojea,
    Kwa maringo kujigamba, hakuna tamfikia,
    Kwanini binadamu, una moyo kama samba?

    Yeye yu sawa na paka, mkia kuuzungusha,
    Na panya atapofika, maisha kumkatisha,
    Kibindoni kumuweka, kapata chakula tosha,
    Kwanini binadamu una moyo kama sumu?

    Yu sawa na mwewe pia, angani kujipitia,
    Sauti nzuri kutoa, vifaranga kuhadaa,
    Na pale taposhukia, wote wataangamia,
    Kwanini binadamu, una moyo kama sumu?

    Zaidi kimwangalia, macho Huruma atia,
    Moyowe kiufikia, kutu umejijazia,
    Upole kajifanyia, apate kukuhadaa,
    Kwanini binadamu, una moyo kama sumu?

    Neon zuri kikwambia, wapaswa kufikiria,
    Kwa hila takuibia, pasipo wewe kujua,
    Na mwisho akukimbia, kikuacha kiteketea,
    Kwa nini binadamu, una moyo kama sumu?

    Hatitamati natia, ujumbe nimeutoa,
    Walo wengi tasikia, wchache tapuuzia,
    Ila rai ninitoa, binadamu jirudia,
    Kwanini binadamu, una moyo kama sumu?

    ReplyDelete
  2. SIKU HII HAPO KESHO (17/10/2010) ngulu

    Siku hii ikifika,
    Wapenzi watakutana,
    Kwa miadi walopeana,
    Ya mapenzi yalofana.

    Siku ilo kama hii,
    Wala sio ya jana,
    Ndiyo siku ya vijana,
    Faraja kutakiana.

    Hii ni siki kuu,
    Ukweli tutauona,
    Na uongo kuukana,
    Tutafanya yalo mana.

    Siku hii ya ajabu,
    Si usiku ni mcchana,
    Vita tutapigana,
    Na ushindi kuuona.

    Hii ni siku gani?
    Siku isiyo na jina,
    Bado hatujaiona,
    Kilamtu anaguna,

    Siku iliyo njema,
    Mwaka huu si mwaka jana,
    Wapenzi watadanganyana,
    Na hatima kutengana.

    Siku tunayoipenda,
    Ndiyo ya kusalitiana,
    Hata tukakosana,
    Na mapanga kukatana.


    Siku itakapofika,
    Tulotenda tayaona,
    Nafsi zitatukana,
    Mtetezi `tutamwona,




    Na siku ikipita,
    Tatamani iwe jana,
    Upendo tuanze peana,
    Kama livyokuwa jana.

    Yenyewe siku ndiyo hii!
    Wakumbuka tuliyoagana?
    Au kwako hayana mana?
    Kama livyo mla jana?!

    Siku hii imeshapita,
    Iweje waniona wa maana,
    Si uliniona dubwana?
    Au pakwenda hauna?

    Siku ilishapita,
    Ya leo haina maana,
    Kwaheri ya kuonana,
    Kijaliwa taonana.

    Siku hiijamani,
    Ni ya kesho sio jana,
    Kama leo tulivyoagana,
    Siku hii hapo kesho.

    ReplyDelete
  3. KUMBUKA

    Nchi imepasuka,
    Vilio vinasikika,
    Hatona pakushika,
    Shida.

    Wanyonge wanateseka,
    Magonjwa yasotibika,
    Wachache wametukuka
    Udhia.

    Binadamu ni wanyama,
    Hawana hata Huruma,
    Wapenda sana hujuma,
    Shida.

    Imani imewatoka,
    Mungu kutomkumbuka,
    Shetani anasifika,
    Udhia.

    Mabaya tunatukuza,
    Mazuri tumepuuza,
    Tunajifanya bazuza,
    Shida.

    Ndugu, imani shika,
    Kumbuka ulikotoka,
    Acha huo ufuska
    Kumbuka.


    ReplyDelete
  4. PEPONI DUNIANI (19/10/10)

    Wametuvisha miwani,
    Miwani ya juani,
    Kutupeleka peponi,
    Peponi duniani.

    Mbona sasa hatuoni?
    Hatuoni yalo mbeleni,
    Giza limo machoni,
    Macho yamo gizani.


    Miwani ya jua gizani?!
    Gizani tusiwabaini,
    Wamebeba vitu pomoni,
    Pomoni bila sisi kubaini.

    Tumepumbazwa akili,
    Akili zikakubali,
    Tukavikwa na bangili,
    Bangili lisilo fahali.

    Sasa nchi I mashakani,
    Mashakani kwa madeni,
    Na wananchi wa vitani,
    Vitani kwa umasikini.

    Hatujafika peponi,
    Peponi ku duniani,
    Tumejiweka motoni,
    Motoni limo shetani.

    ReplyDelete
  5. NDOTO NJEMA (10/10/10)

    Kaa chini mwanangu,
    Nikufugulie moyo wangu,
    Uione ndoto yangu,
    Ipokee.

    Wala usishituke,
    Ila akilini iweke,
    Ina umuhimu wake,
    Sikia.

    Ila usije kusema,
    Usije umwaga mtama,
    Kwa hili ninalosema,
    Elewa.

    Shuleni unakokwenda,
    Utayapata matunda,
    Watu watakupenda,
    Amini.

    Upendo ni chako kipawa,
    Huruma umejaliwa,
    Ugomvi hukutupiwa,
    Hakika.

    Siku ikifika,
    Hatamu utaishika,
    Na utakubalika,
    Ni kweli.

    Wanyonge utatetea,
    Taifa takutegemea,
    Ndiyo ndoto nakwambia,
    Ndoto njema.



    Kibwagizo;
    Wote tumwombe Mungu,
    Atuondolee ukungu,
    Tutende ya kiungu,
    Anina.

    ReplyDelete
  6. NI WEWE (19/10/10)

    Si wewe!
    Uliyeniahidi,
    Utanitoa baridi,
    Sasa wanifisidi,
    Kwanini?

    Si wewe!
    Tuliopanga kalenda.
    Ya raha kuziponda,
    Leo unanitenda,
    Kwanini?

    Si wew!
    Uliyeapa milele,
    Nami kusonga mbele,
    Leo wapiga misele,
    Kwanini?

    Si wewe!
    Uloniachisha shule,
    Nilipogongewa kengele,
    Nina mamba ya Sele,
    Kwanini?

    Si wewe!
    Ulomkana mwanangu,
    Na kunipiga majungu,
    Ukanitia uchungu,
    Kwanini?

    Si wewe!
    Nilokupa kura yangu,
    Uiokoe nchi yangu,
    Sasa umetugawa mafungu,
    Kwanini?

    Si wewe!
    Uloua wazazi wangu,
    Ukaninyang`anya mali zangu,
    Na kuwatesa ndugu zangu,
    Kwanini?



    Si wewe!
    Unayelinda nchi yangu,
    Mbona watesa watu wangu,
    Unawafunga kwa pingu,
    Kwanini?

    Si wewe!
    Tulopanga kuungana,
    Umoja uliofana,
    Leo unanikana
    Kwanini?

    Si wewe
    Si! tulopanga kupigana,
    Kuwakomboa wetu wana,
    Leo wanitukana
    Kwanini?

    Si wewe!
    Uliye waua walemavu,
    Wa ngozi kwa mabavu,
    Kwa sababu ya wivu,
    Kwanini

    Siwewe!
    Uliyenisaliti,
    Ukanifanya mauti,
    Kwa kuzipenda noti,
    Kwanini?

    Ni wewe!
    Usiyekuwa na utu,
    Umejitia kutu,
    Hauwathamini watu,
    Ni wewe!

    ReplyDelete
  7. AHADI

    ‘Its my promises’
    Sauti iliyotoka,
    Katika simu niliyoshika,
    Ni mbali ilipotoka,
    Ahadi.

    Ahadi ikasikika,
    Kichwani ikashikika,
    Mtima ukapasuka,
    Si utani si mahoka,
    Ni ahadi.

    Ya penzi kulienzi,
    Kwa ufundi na ujuzi,
    Pasi kuleta majonzi,
    Kwangu mie wake mwenzi,
    Naomba.

    Ee Mungu uliyetukuka,
    Kati yako na malaika,
    Ahadi ninaiweka,
    Daima sitakiuka,
    Nijalie.

    Pendo liwe la ambari,
    Zinduna na saburi,
    Pasi chuki na kiburi,
    Uhasidi na jeuri,
    Tujalie.

    Tupendane kwa makeke,
    Katu pendo lisishuke,
    Awe wangu niwe wake,
    Hadi mauti `tufike,
    Tufe wote.

    ReplyDelete
  8. KUMWAGA CHOZI SI UTOTO (20/10/10)

    Nlipokuwa motto, sikulibaini hili,
    Mtu kupata majuto, ni kuikosa kauli,
    Sasa nina wangu wito, na pia ninakubali,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    Wengi walilia sana, kuyakumbuka ya jana,
    Walivyo furahi sana, wakachezea ujana,
    Nafsizo zawakana, akili zawalumbana,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    Na wapo wanaolia, kuwapoteza wazazi,
    Wale waloangamia, kwa matukio ya wizi,
    Dunia mewalemea, kwa kukosa mtetezi,
    Mtu kulimwaga chozi hakika sio utoto.

    Lo! Wapo wanaolia, kukosa walivyopenda,
    Huzuni mewazoea, `wajawahi onja tunda,
    Majuto ni yao njia, popote wanapokwenda,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    Wengine pia hulia, kuvipoteza viungo,
    Ni chungu kwao dunia, uchungu usio kingo,
    Ajali waliumia, wakavunjika mgongo,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    Vita vinavyo rindima, ni wanyonge wateseka,
    Mabomu sasa yasema, na bunduki kadhalika,
    Amani imetuhama, nchi sasa inanuka,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    Masikini chetu cheo, kila mtu atucheka,
    Hatuujui uchao, na uchwao si hakika
    Wachache ni wala vyao, wengi tunasulubika,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    Lakini tafika siku, na sisi kupata utu,
    Si mchana si usiku, hatamu takuwa yetu,
    Tusahau ukasuku, tufurahi na wanetu,
    Mtu kulimwaga chozi, hakika sio utoto.

    ReplyDelete
  9. NCHI YANGU

    Daima najivunia,
    Kuwa mtanzania,
    Wala sitopuuzia,
    Uovu nitakimbia,
    Amani kuitakia,
    Kazi kufanya pia,
    Uchumi kujikuzia,
    Hiyo ndiyo yangunia,
    Dua ninaiombea,
    Migogoro kuepushia,
    Mungu unipe nia,
    Niipende bila kina,
    Nchi yangu Tanzania.


    ReplyDelete
  10. NI RADI AU TUFANI?

    Kichwa changu chaniuma, mawazo tele kujaza,
    Siwezi hata kusema, ni kipi nacho kiwaza,
    Nashindwa hata kuhema, wala sauti kupaza,
    Ukimwi ni kitu gain, ni radi au tufani?

    Chanzo chake sijajua, wapi ulipoanzia,
    Hata kwetu kuingia, mwishowe ukaenea,
    Wenzetu umechukua, kumi elfu mamia,
    Ukimwi ni kitugani, ni radi au tufani?

    Unasambazwa kwa ngono, tena isiyo salama,
    Na wala si kwa mkono, jinsi wengi wanasema,
    Lingine ni kwa mdomo, penzi mnapopeana,
    Ukimwi ni kitu gain, ni radi au tufani?


    Vitu vyenye ncha kali, vyaweza kutupatia,
    Wembe, pini si halali, pamaja kuvitumia,
    Sindano itupe mbali, au shimoni fukia,
    Ukimwi ni kitugani, ni radi au tufani?

    Mgonjwa kupewa damu, maisha kuyaokoa,
    Kumbe damu ina sumu, gonjwa mmempatia,
    Ni vyema kuihukumu, mgonjwa kutofikia,
    Ukimwi ni kitugani, ni radi au tufani?

    Mama kwenda kwa motto, hiyo yaweza changia,
    Pia yaleta majuto, kwa kiumbe kisojua,
    Anyonyeshwavyo motto, virusi humuingia,
    Ukimwi ni kitu gani, ni radi au tufani?

    Dalili zake ni nyingi, chache nitawatajia,
    Kutokwa na mashilingi, mwili kudhoofu pia,
    Homa zisizo msingi, kilasiku kurudia,
    Ukimwi ni kitu gani, ni radi au tufani?

    Hasirazo humjia, mgonjwa akigundua,
    Akilize humtuma, uhai kuutimua,
    Wenzake kuwakibia, hataki kuwasikia,
    Ukimwi ni kitu gani, ni radi au tufani?


    ReplyDelete
  11. JUA

    Jua twafahamu si sayari,
    Hucomoza mashariki,
    Na kuzama magharibi,
    Hii ni kama sheria.

    Jua hutoa Mwanga,
    Njia kutumulikia,
    Twendapo kutopotea,
    Malengo kuyafikia.

    Jua hutoa vitamini,
    Mwili kuupa madini,
    Matege kuweka pembeni,
    Afya zilizo makini.


    Jua latupa umeme,
    Njumbani kuutumia,
    Wanafunzi twasomea,
    Hospitalini tiba pia.

    Chakula hutengeneza,
    Mimea husheheneza,
    Rutuba tele kujaza,
    Yastawi kwa furaha.

    Lakini najua JUA,
    Ni kufahamu pia,
    Kitu kukitambua,
    Zaidi kung`amua.

    Jua ni kitu kizuri,
    Tena kilo thamani,
    Ukiwekapo ndani,
    Fahari wajivunia.

    Kuwa nalo napata hamu,
    Furaha iliyo adimu,
    Maisha sio magumu,
    Kwa wake Mwanga nadumu.

    Kwangu wewe muhimu,
    Maisha kwangu udumu,
    Wasijenipa hukumu,
    Wale wakaanga sumu.

    Jua nakuombea,
    Shairi kukuibia,
    Na muda kuutumia,
    Amani kukutakia.

    Uliyopanga kutimia,
    Mwanasheria kufikia,
    Kama ulivyo ahidia,
    Wanyonge kuwatetea.

    Mungu awe daima kwako,
    Na autunze moyo wako,
    Azidishe imani yako,
    Mafanikio yawe maishani mwako,
    AMINA

    ReplyDelete
  12. MWANAFUNZI

    Mwanafunzi nakujia,
    Wosia kukupatia,
    Masomo kuzingatia,
    Malengo kuyafikia.

    Unapokuwa darasani,
    Sikiliza kwa makini,
    Tachofundishwa baini,
    Ukiweke akilini.

    Heshima kitu muhimu,
    Walimu uwaheshimu,
    Kwa wenzako ni muhimu,
    Ili amani idumu.

    Umoja ndicho kigezo,
    Kwa wenye na waso uwezo,
    Utakuwa ndiyo nguzo,
    kukupa wewe mwongozo.

    Ugumu napobaini,
    Zidisha yako makini,
    Waombe walo jirani,
    Msaada wao jamani.

    Kiburi si maungwana,
    Majivuno na kujiona,
    Kwa wenzako changamana,
    Mazuri utayaona.

    Mahusiano ya mapenzi,
    Yadumaza wako ujuzi,
    Ukimuwaza wako mwenzi,
    Wenzako wapiga mbizi.

    Pia ni hatari sana,
    Kwa mimba bado kijana,
    Kumbuka ya mwaka jana,
    Aliacha masomo Amina.

    Magonjwa wawezapata,
    Kwa huko kupitapita,
    Achana na huyo Pita,
    Malengo yo tayafuta.

    Kumbuka ulikotoka,
    Mawazo akilini weka,
    Wazazi walijitwika,
    Msalaba ili usome.

    Mchezo kabisa acha,
    Uchochoroni kujificha,
    Na mibangi kuivuta,
    Hakuna takachopata.

    Kumbuka wadogo zako,
    Nyumbani huko walipo,
    wategemea msaada wako,
    usome uwaokoe.

    Wakumbuke baba na mama,
    Uzee wawasakama,
    Hawana nguvu kulima,
    Tegemeo kwako mjomba.

    Kumbuka baraka njema,
    Shuleni tunakutuma,
    Huko waenda kusoma,
    Ukasome mwanetu soma.

    Ukishatoka masomoni,
    Uje tutoa shimoni,
    Umasikini hatuutamani,
    Wewe ni wetu rubani.

    Wahenga walisawili,
    Kuwa akili ni mali,
    Soma upate akili,
    Maisha kuyakabili.

    Zaidi walibaini,
    Kuwa mchumia juani,
    Kivuno hula kivulini,
    Kwa raha na amani.

    Masomo ukichezea,
    Kaburi wajichimbia,
    Wahenga walitwambia,
    Ni ngumu hii dunia.

    Machungu takujia,
    Dunia takulemea,
    Mwishowe utajutia,
    Masomo kuyachezea.

    Yote kasha kumbuka,
    Aibu itakufika,
    Kwa wako huo ufuska,
    Masomo kutoyashika.

    Hapa mwisho nakita,
    Nisijeleta matata.
    Matatizo nikayapata,
    Nikakosa nilikchofuata.

    ReplyDelete

Thank for your coment

Powered by Blogger.